Alama yako ya Ustawi wa Akili ni ipi?

Chukua kipimo cha MHQ kufahamu.
Ni cha siri na huchukua dakika 15 au chini ya hapo.

Anza

What is your Mental Wellbeing Score
Badilisha Lugha

Lazima uwe na umri wa miaka 18 au zaidi ili kuchukua tathmini hii. Hatukusanyi taarifa yoyote nyeti iwezayo kumtambulisha mshiriki. Unaweza kusoma sera yetu ya faragha hapa. Jibu lako litakuwa sehemu ya Mradi wa Akili Kimataifa, na hivyo kutoa taswira juu ya ustawi wa akili wa idadi ya watu duniani.

USTAWI WA KIAKILI NI NINI NA MHQ INAKUAMBIA NINI?

Ustawi wa akili ni uwezo wa kushughulikia maisha na mifadhaiko na changamoto zake mbalimbali. Kwa hivyo MHQ ni taswira ya mtazamo wako binafsi katika nyanja mbalimbali za utendakazi wa akili ambazo huamua ustawi wako wa kiakili. Si kipimo cha furaha au kuridhika kimaisha. Unaweza, kwa mfano, kuwa unapitia hali ngumu sana au za kusikitisha maishani mwako lakini hata hivyo ukawa na uwezo wote wa kuzistahimili kadri iwezekanavyo, na hivyo kuwa na kiwango cha juu cha ustawi wa akili.

ALAMA NA RIPOTI YAKO YA MHQ

82

Alama ya Jumla ya MHQ

MHQ itakupatia kiautomatiki alama ya jumla ya afya ya akili utakapokamilisha kujibu maswali yote. Unaweza pia kuomba kupatiwa ripoti ya hiari iliyo na unyumbuisho wa alama katika vipimo sita vya afya ya akili pamoja na maelezo na mapendekezo, kwa kutoa barua pepe yako.

Alama katika vipimo 6 vya afya ya akili

Vipimo Sita vya Afya ya Akili Katika MHQ

Mood and Outlook

Hisia na Mtazamo wa Kifikra: Uwezo wako wa kusimamia na kudhibiti hisia zako kwa ufanisi na kuwa na mtazamo mzuri au wenye matumaini kwa siku zijazo.

Social Self

Taswira Binafsi Kijamii: Jinsi unavyoshirikiana, kuhusiana na kujiona ukijilinganisha na wengine.

Drive and Motivation

Msukumo wa Ndani na Motisha: Uwezo wako wa kufanya kazi ili kufikia malengo yako unayotaka na kuanzisha, kudumisha na kukamilisha shughuli zilizopo katika maisha yako ya kila siku.

Cognition

Ufahamu: Uwezo wako wa kufanya shughuli za msingi za ufahamu, kuelewa changamano tete za matukio na hali, na kuonyesha kuzingatia mtazamo wa muda mrefu katika mawazo na tabia yako.

Adaptability & Resilience

Kukabiliana na Hali & Ustahimilivu: Uwezo wako wa kubadilisha tabia na mtazamo wako ili kukabiliana na mabadiliko ya hali na kukabiliana na changamoto na vikwazo unavyokutana navyo.

Mind-Body Connection

Uhusiano wa Akili na Mwili: Udhibiti wa usawa kati ya akili na mwili wako.

Alama yako ya MHQ