Katika namna tusiyoweza kuielewa kikamilifu, ustawi na uwezo wa akili zetu kufanya kazi, hubadilika kadri mazingira yetu ya kijamii, kiteknolojia na kitamaduni yanavyobadilika. Mradi wa Akili Kimataifa unalenga kufuatilia na kuelewa uhusiano huu unaoonekana kupitia mageuzi, ili kuweza kuandaa vyema mustakabali wa afya na ustawi wa jamii zetu.

Mental Health

Mradi wa Akili Kimataifa hutumia majibu ya tathmini ya MHQ, yatolewayo bure pasipo utambulisho na hutoa ripoti kupitia barua pepe iainishayo alama na mapendekezo mahsusi.

Shiriki

MRADI

Mradi huu umetengeneza hazinadata kubwa zaidi duniani yenye taarifa za kina kuhusiana na afya ya akili sambamba na vichochezi vinavyosababishwa na idadi ya watu, mitindo ya maisha na hali za maisha za watu watumiao intaneti.

Data hizi hutumika:

  • Kujenga taswira ya ustawi na uwezo wa utendaji kazi wa watu, na mataifa yaliyopo kote ulimwenguni.
  • Kuelewa visababishi vikuu vya mwenendo uliopo wa kuzorota kwa afya ya akili.
  • Kutoa suluhisho la kuzuia hali hii, litakalobadili mwelekeo wa hali ya afya ya akili.

HAZINADATA

Hazinadata sasa inajumuisha taarifa za zaidi ya watumizi milioni 1 wa intaneti kutoka zaidi ya nchi 71 na katika lugha 14, sambamba na vichochezi vya idadi ya watu, mitindo na hali za maisha. Zaidi ya taarifa za watu 2000 wapya huongezwa kila siku. Ni usanifu madhubuti na mwepesi uwezeshao uchunguzi wa haraka wa mienendo inayoibuka.

TUSAIDIE KUTIMIZA MALENGO YETU

Mradi wa Akili Kimataifa ni harakati isiyo ya kimaslahi na tunategemea usaidizi wako utusaidie kufikia hadhira kubwa zaidi na kufanya matokeo yapatikane kwa wingi zaidi kwa umma na watunga sera.

Take Part

SHIRIKI

Chukua kipimo cha MHQ ili kuongeza wasifu wako wa afya ya akili kwenye hifadhidata, pasipo kujulikana.
SHIRIKI

Partner

MSHIRIKA

Wasiliana nasi ili kupima na kuwakilisha ustawi wa kiakili wa jamii zako.
MSHIRIKA

Donate

CHANGIA

Tusaidie kufikia malengo yetu ya kukusanya taarifa na kuunda taswira za taarifa ili kushirikisha matokeo.
CHANGIA