Blogu

Therapist giving advice

Alama Hasi ya MHQ ni Ishara Inayokutaka Kutafuta Usaidizi wa Kimatibabu

Alama hasi ya MHQ huashiria hali mbaya ya afya ya akili. Haya ndio mambo ya kufahamu na jinsi ya kupata usaidizi.

Alama hasi kwenye MHQ (Kiwango cha Afya ya Akili) huashiria kwamba unaweza kuwa unakabiliana na, au kuwa katika hatari ya, hali mbaya ya afya ya akili. Ikiachwa bila kudhibitiwa, hali hii inaweza kusababisha matokeo mabaya kimaisha, na hata kuweza kusababisha kifo. Ni muhimu kutafuta msaada. Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazoweza kusababisha alama hasi ya ustawi wa akili:

  • Hali ya kinasaba inayoathiri utendakazi wako
  • Athari mbaya za dawa
  • Tatizo la neurolojia
  • Matokeo ya ajali, kama vile jeraha la kichwa
  • Kiwewe cha Maisha

Haya ni baadhi tu ya masuala yanayoweza kusababisha alama hasi. Hata hivyo, mtaalamu afanyaye utathmini kikamilifu ndie pekee anayeweza kusema kwa uhakika.

Ni muhimu kutafuta msaada wa kimatibabu

Mara nyingi, mtaalamu wa afya ya akili mwenye sifa huweza kukusaidia kudhibiti, kubadilisha au kuondoa matatizo. Hata hivyo, hata pale wanapofahamu matatizo makubwa, watu wengi huwa hawamtembelei mhudumu wa afya ya akili hata kidogo, labda kutokana na hofu, uepukwaji, unyanyapaaji, au ukosefu wa rasilimali. Kihalisia, 44% ya watu waliopo katika kundi la mfadhaiko au tatizo, hutoa taarifa kwamba, hawajaomba kupatiwa usaidizi kokote. Kwa bahati mbaya, hili humaanisha kuwa changamoto zinaweza kuwa mbaya zaidi kadri muda unavyokwenda.

Changamoto za kufadhaisha za afya ya akili zinaweza kudhoofisha na mara nyingi huhitaji suluhisho mbalimbali pamoja na usimamizi endelevu. Kinachofaa kwa mtu mmoja huenda kisifanye kazi kwa mwingine. Hata hivyo, wengi hujionea kwamba, kupata usaidizi wa kimatibabu ni jambo linalostahili jitihada zao. Nchini Marekani, zaidi ya 40% ya watu wamekwishawahi kujipatia ushauri nasaha, na mtu mmoja kati ya watu sita hutumia aina fulani ya dawa za akili. Watu wengi wamekubaliana kwamba si kila mara tutaweza wenyewe kujipatia unafuu. Hizi ni baadhi ya njia ambazo usaidizi wa kitaalamu unaweza kuleta mabadiliko:

  1. Kuzuia matatizo. Baadhi ya masuala ya afya ya akili yanaweza kukua na kupelekea masuala ya uraibu, tabia za kujiua, hasira au kujitenga. Mtaalamu mwenye sifa hufahamu maeneo haya na huweza kusaidia kutibu au kuzuia matatizo.
  2. Utambuzi wa hali ya kiafya. Kama ilivyoelezwa, wakati mwingine masuala ya afya ya akili yanaweza kusababishwa na hali ya kimwili. Kutambua msingi wa tatizo na kulishughulikia kunaweza kuokoa maisha.
  3. Kuboresha ubora wa maisha. MHQ hasi huenda ikapima kile ambacho tayari unakijua-kwamba maisha yanaweza kuwa magumu. Hali hii inaweza kufanywa kuwa ngumu zaidi kutokana na matukio ya hivi karibuni ulimwenguni. Mhudumu wa afya ya akili mwenye sifa anaweza kukusaidia kutibu, kudhibiti au hata kuondoa baadhi ya matatizo ya akili. Hii mara nyingi husababisha kuboreshwa kwa mahusiano, kuridhika kwa maisha, na kuongezeka kwa uwezo wa kutambua na kufikia malengo ya maisha.

Tazama machapisho yanayohusiana – Kuelewa Hisia na Mtazamo na Taswira binafsi kijamii ni nini?

Ishara za Tahadhari Zinazohitaji Usaidizi wa Haraka

Ingawa kutafuta daktari au mshauri ni ufunguo wa kushughulikia masuala ya afya ya akili, kuna hali baadhi ambazo hupaswi kusubiria miadi, na badala yake utapaswa kuchukua hatua mara moja. Hali hizi ni pamoja na:

  • Mabadiliko ya ghafla katika hali ya akili. Ikiwa umegundua mabadiliko ya hivi karibuni au ya ghafla katika hali ya akili, au wengine wameona na kukuambia kuhusu hilo, unapaswa kupiga simu kwa daktari wako au kwa huduma za dharura mara moja. Hii inaweza kuwa ishara ya tahadhari ya jambo zito zaidi, ila kutafuta msaada mara moja kunaweza kuleta tofauti.
  • Mawazo ya kujiua au kujidhuru. Ikiwa umekuwa ukifikiria kujidhuru au kujiua, hauko peke yako. Watu wengi hupata mawazo haya, hata hivyo, hiki sio kitu cha kukishughulikia peke yako. Wasiliana na huduma za dharura za eneo lako, au tembelea hapa ili kuwasiliana na Huduma ya Kuzuia Vitendo vya Kujiua. Unapaswa pia kuwasiliana na daktari wako, mtaalamu wa tiba, au huduma nyingine za afya ya akili katika eneo lako ili kupata usaidizi wa muda mrefu.
  • Mawazo ya kuwadhuru wengine. Sawa na mawazo ya kujiua, baadhi ya watu mara kwa mara huwa na mawazo ya kutaka kuwadhuru wengine. Hii pia inaweza kuwa ishara ya ugonjwa wa akili, au hata kuashiria uwepo wa athari ya dawa, na unapaswa kuwasiliana na daktari wako au mtaalamu wa ndani mara moja ili kupata msaada wa kukabiliana na hali hiyo. Ikiwa umeweka mpango wa haraka wa kumdhuru mtu, wasiliana na huduma za dharura zilizopo karibu nawe.

Njia za Kupata Msaada wa Kitaalamu

Endapo kama hautakuwa katika hatari ya haraka, basi hatua itakayofuata ni kuweka miadi ya matibabu. Hizi ni chaguzi chache unazoweza kuchagua:

  • Zungumza na daktari wako wa huduma ya msingi. Daktari wako anaweza kutathmini hali yako, kutibu hali na hatari za kimwili, na kukuelekeza kwa mtaalamu anayefaa.
  • Weka miadi ya kuonana na mtaalamu wa magonjwa ya akili. Madaktari wa magonjwa ya akili na wataalamu wengine wa matibabu wenye sifa wanaweza kukuagizia dawa ikiwa inafaa, au kukuelekeza kwa mtaalamu mwingine. Hali hii inaweza kukutisha, lakini kumbuka, nchini Marekani pekee mtu mmoja kati ya sita humeza dawa za akili, kwa hiyo hali hii ni kawaida, na inaweza kuleta tofauti kubwa. Unaweza pia kuchunguza chaguzi za matibabu ya akili mtandaoni, kama vile matibabu ya akili kupitia teknolojia ya mawasiliano mtandaoni, yaliyo ya gharama nafuu zaidi.
  • Weka miadi ya kupatiwa matibabu. Wataalamu wengi wa tiba huweza kutoa tathmini kamili ya afya ya akili na ama kukusaidia na mpango wa matibabu au kukuelekeza kwa daktari au mshauri maalumu.

Ikiwa huna uwezo wa kufikia wataalamu wa ndani, unaweza kupata msaada kupitia huduma za simu. Nchini Marekani, unaweza kupiga simu kwa SAMHSA (Idara ya Huduma za Afya ya Akili na Udhibiti wa Matumizi Mabaya ya Dawa) katika nambari 800-662-4357.

Ingawa kutafuta msaada linaweza kuwa jambo la kuogopesha, tambua kwamba hauko peke yako, na kwamba kuchukua hatua sasa kunaweza kuboresha maisha yako.