Sera ya Faragha

Ilibadilishwa mwisho: Mei 4, 2020

Sapien Labs ni shirika la utafiti lisilo la kimaslahi lenye dhamira ya kuelewa na kuwezesha akili ya binadamu. Wakati mwingine, tunaweza tukahitaji kukusanya taarifa kuhusu watumiaji wetu na matumizi yao ya tovuti yetu ili kutusaidia kufikia lengo hilo.

Sera hii ya faragha (“Sera ya Faragha”) inafafanua jinsi tunavyotumia, tunavyoshirikisha, na tunavyolinda taarifa tunazokusanya kutoka kwako kupitia tovuti, programu, au huduma za mtandaoni ambazo Sapien Labs inaendesha au zinazounganishwa na Sera hii ya Faragha (kwa pamoja, “Huduma”). Sera hii ya Faragha hutumika tu katika Huduma.

Tafadhali zingatia kwamba sera tofauti ya faragha inaweza kutumika kwenye huduma za wahudumu wengine unaowatumia kufikia maudhui yetu. Zaidi ya hayo, ikiwa tutafanya utafiti, tunaweza kufanya hivyo kwa mujibu wa makubaliano tofauti, kwa hivyo Sera hii ya Faragha haiwezi kudhibiti uchakataji wa taarifa zitakazotokana na utafiti huo. Tunakuhimiza sana kujitahidi kuelewa si tu Sera hii ya Faragha, lakini pia sera zingine zozote za faragha au makubaliano yanayoweza kudhibiti matumizi yako ya huduma.

Taarifa tunazokusanya

Maelezo ya mawasiliano. Baadhi ya fomu na huduma huuliza jina na anwani yako ya barua pepe ili kukupatia taarifa unayoomba.

Maswali ya utafutaji kwenye mtanda. Huduma zetu zinaweza kujumuisha maeneo yanayokuruhusu kutafuta (katika maeneo ya huduma yetu tu) maudhui au majibu ya maswali. Tunakusanya taarifa kuhusu vitu na mada unazoziulizia, na hoja zozote za ziada katika utafutaji kwenye mtandao.

Maudhui yako. Tunakusanya maoni na maelezo mengine unayochapisha kupitia vipengele shirikishi vya mtandaoni. Hata hivyo, taarifa zote kama hizo huandaliwa kabla au kuboreshwa ili kuepuka kukusanya taarifa binafsi na kusaidia kudumisha mazingira salama kwa watumiaji.

Taarifa za Mawasiliano. Tunaweza kuhifadhi taarifa za mawasiliano baina yetu na wewe zinazohusiana na huduma zetu.

Matumizi ya Huduma. Tunaweza kuhifadhi taarifa kuhusiana na jinsi Huduma zetu zinavyotumiwa.

Maelezo ya kifaa. Tunaweza kukusanya taarifa kuhusu kifaa chako, ikijumuisha muundo wa maunzi, toleo la mfumo wa uendeshaji na vitambulishi vya kipekee.

Tunatumia taarifa tunazokusanya ili…

  • Kusaidia kukupa maudhui na huduma muhimu zaidi
  • Kutuma nyenzo za utangazaji, au nyenzo zingine zinazohusiana na huduma zetu;
  • Kuchanganua matumizi ya Huduma ili kuelewa, kuendeleza na kuboresha Huduma zetu, kama vile kubainisha kurasa zinazojulikana zaidi, vivinjari vinavyotumiwa zaidi, muda ambao watumiaji hutumia kwenye Huduma, na tovuti wanazotoka;
  • Vinginevyo husaidia utendakazi wa ndani wa Huduma;
  • Kukupatia taarifa kulingana na wajibu wetu wa kisheria, ikiwa ni pamoja na katika tukio la utumiaji mbaya wa taarifa;
  • Kuzuia shughuli zilizopigwa marufuku au haramu, na kushinikiza Vigezo vya Utumiaji; na
  • Kwa ajili ya madhumuni mengine yoyote yatakayobainishwa kwako wakati tunapokusanya taarifa au kwa mujibu wa idhini yako.

Kushirikisha taarifa na wahusika wengine

Tunaweza kushirikisha taarifa iliyokusanywa kutoka kwako kama ifuatavyo:

  • Watu wengine walioidhinishwa. Tunaweza kushirikisha taarifa kwa watu wetu wengine ambao hutusaidia kuwasilisha maudhui na huduma zetu.
  • Hamisho za ki-biashara. Tunaweza kushirikisha taarifa inayohusiana na miamala mikubwa ya kibiashara, kama vile uuzaji wa Huduma, muunganisho, ujumuishaji, uuzaji wa mali, au katika tukio lisilotarajiwa la kufilisika.
  • Madhumuni ya kisheria. Hatukodishi au kuuza taarifa kwa wahusika wengine, lakini tunaweza kuweka wazi taarifa ili kujibu wito, amri za mahakama, mchakato wa kisheria, maombi ya kutekeleza sheria, madai ya kisheria au maswali ya serikali ili kulinda na kutetea haki zetu, maslahi, mali, usalama na ulinzi.

Jinsi tunavyokusanya taarifa

Tunaweza kutumia javascript, vidakuzi, vinara vya wavuti, Vitu Vilivyoshirikishwa vya Karibu Nawe (local shared Objects), na teknolojia zingine kama hizo kukusanya taarifa kuhusu matumizi yako ya Huduma. Vitu Vilivyoshirikishwa vya Karibu Nawe (wakati mwingine hujulikana kama “vidakuzi vya Adobe Flash”) hupakuliwa kwenye kompyuta au kifaa cha rununu na kicheza media cha Adobe Flash.

Tunatumia teknolojia hizi kupima, kuchanganua na kuboresha Huduma zetu. Kwa mfano, tunatumia teknolojia hizi ili kutusaidia kutambua kivinjari chako kama mtumiaji wa awali na kuhifadhi mapendeleo yoyote ambayo yanaweza kuwa yamewekwa ili kutusaidia kubinafsisha maudhui yanayoonyeshwa unapotumia Huduma; kukupa maudhui yaliyobinafsishwa kulingana na mapendeleo yako; kuelewa kama unasoma jumbe za barua pepe na kubofya viungo vilivyomo ndani ya jumbe hizo, ili tuweze kuwasilisha maudhui na matoleo muhimu; na kusaidia kupima na kutafiti ufanisi wa Huduma zetu.

Tunaweza kuruhusu wahusika wengine kuweka na kusoma vidakuzi vyao wenyewe, vinara vya wavuti, na teknolojia sawa na hizo ili kukusanya taarifa kupitia Huduma pamoja na kutusaidia kupima wingi wa watumiaji wa tafiti na vichambuzi. Tunawaruhusu wahusika hawa wengine kukusanya taarifa ya vidakuzi na vitambulishi vinavyofanana navyo, ambavyo havikutambulishi moja kwa moja.

Unaweza kukataa au kuzima vidakuzi kwa kurekebisha mipangilio ya kivinjari chako cha wavuti. Kwa sababu kila kivinjari cha wavuti ni tofauti, tafadhali soma maelekezo yaliyotolewa na kivinjari chako cha wavuti (kawaida katika sehemu ya “msaada”). Tafadhali kumbuka kuwa unaweza ukahitaji kuchukua hatua za ziada ili kukataa au kuzima Vitu Vilivyoshirikishwa vya Karibu Nawe (Local Shared Objects) na teknolojia zinazofanana navyo. Kwa mfano, Vitu Vilivyoshirikishwa vya Karibu (Local Shared Objects) vinaweza kudhibitiwa kwa kufuata maelekezo yaliyopo kupitia maagizo kwenye ukurasa wa Kidhibiti cha Mipangilio ya Adobe. Iwapo utachagua kukataa, kuzima, au kufuta teknolojia hizi, basi baadhi ya utendaji kazi wa Huduma zetu unaweza usipatikane kwako tena.

Kuhusu mifumo ya mawimbi yaondoshayo ufuatiliaji ya usifuatilie na taratibu zinazofanana nayo: Baadhi ya vivinjari vya wavuti husambaza mawimbi ya “usifuatilie” kwenye tovuti. Kutokana na tofauti ya jinsi vivinjari hujumuisha na kuwezesha kipengele hiki, si mara zote huwa bayana kama watumiaji hunuia kutuma mawimbi haya, au hata kama wanafahamu. Kwa sasa hatuchukui hatua yoyote kukabiliana na mawimbi haya.

Matumizi ya mjumuisho wa taarifa

Tunaweza kujumlisha taarifa zako na taarifa za watumiaji wengine kwa njia ambayo haikutambulishi moja kwa moja.

Pia tunaweza kushirikisha taarifa iliyojumuishwa au isiyoweza kutambuliwa na watu wengine, kwa ajili ya madhumuni yanayojumuisha kutusaidia kukuza, kuchanganua na kuboresha maudhui na Huduma. Kuna uwezekano kwamba watu wengine wanaweza kutumia taarifa hii iliyojumuishwa au isiyoweza kutambuliwa na wengine ili kutengeneza kazi na matoleo ya huduma zao.

Kulinda taarifa tunayokusanya

Tumeazimia kulinda taarifa yako. Tumechukua hatua zinazokubalika za kiufundi, kiusimamizi na za kifizikia ili kusaidia kulinda taarifa hizi dhidi ya upotevu, na matumizi mabaya kama inavyofaa, ikiwa ni pamoja na matumizi ya usimbaji fiche. Tafadhali zingatia kuwa hakuna usafirishaji au uhifadhi wa taarifa unaoweza kuhakikishiwa kuwa salama 100%. Tunataka utumie Huduma zetu kwa kujiamini, hata hivyo hatuwezi kukuhakikishia au kukuthibitishia usalama wa taarifa yoyote unayotuma kwetu.

Taarifa kwa watumiaji wa kimataifa

Huduma hizi zimeundwa kwa ajili ya na kulenga hadhira za Marekani, na zinasimamiwa na kuendeshwa kwa mujibu wa sheria za Marekani. Hatutoi madai yoyote ya kuwa Huduma hizi zinaendeshwa kwa mujibu wa sheria au kanuni za mataifa mengine yoyote. Taarifa zinazokusanywa kupitia Huduma hizi zinaweza kuhifadhiwa na kuchakatwa nchini Marekani au ndani ya nchi nyingine yoyote yenye ofisi inayoendeshwa na sisi au watoa huduma wetu. Watoa huduma wetu wanaweza kuhamisha taarifa zako tunazokusanya, zinazoweza kujumuisha taarifa binafsi, kutoka mpaka wa nchi na kutoka kwenye nchi au eneo lako la mamlaka hadi kwenda nchi au maeneo ya mamlaka nyingine, ambayo baadhi yao yanaweza yasiwe na sheria za ulinzi wa taarifa zinazofanana na zile za mamlaka ya eneo lako. Kwa kutumia Huduma hizi na kwa kutupatia taarifa kwa njia ya moja kwa moja au isiyo ya moja kwa moja, unakubali uwepo wa uhamishaji wa taarifa kwenda Marekani ama kwenda nchi nyingine yoyote ambayo watoa huduma wetu huendesha ofisi za uchakatwaji wa taarifa kulingana na Sera hii ya Faragha.

Mabadiliko ya Sera hii ya Faragha

Tunaweza kurekebisha Sera hii ya Faragha, kwa mfano, tunaweza kufanya hivyo ili kuakisi mabadiliko katika sheria, desturi zetu au vipengele vya Huduma. Mabadiliko yasiyo ya nyenzo yataanza kufanya kazi mara baada ya kuchapishwa, hata hivyo daima tutaainisha wazi tarehe ya kuanza kwa mabadiliko kama hayo juu ya Sera hii ya Faragha. Tafadhali pitia Sera hii ya Faragha mara kwa mara ili upate taarifa kuhusu sera na desturi zetu za hivi karibuni zaidi.

Maswali kuhusu Sera hii ya Faragha

Ikiwa una maswali tafadhali wasiliana nasi kupitia:
Sapien Labs
info@sapienlabs.org